Ethiopia yatuhumiwa kuwanyonga wanajeshi wa Sudan


Jeshi la Sudan limeshutumu jeshi la Ethiopia kwa kuwanyonga wanajeshi saba wa Sudan na raia mmoja waliokuwa mateka.


Taarifa iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari vya serikali ya Sudan haikutoa maelezo zaidi.


Lakini iliyaita mauaji hayo yanayodaiwa kuwa ya kisaliti, na ikasema itazungumza.


Hakujawa na maoni hadi sasa kutoka kwa upande wa Ethiopia.


Mzozo wa muda mrefu wa mpaka umepamba moto katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na mapigano ya hapa na pale katika eneo la al-Fashaga yameshuhudiwa.


Sudan pia imekasirishwa na ujenzi wa Ethiopia wa bwawa kubwa kwenye Mto Nile.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu