Deni la Serikali laongezeka kwa asilimia 13.7Deni la Serikali Tanzania limeongezeka kutoka Sh56.76 trilioni mwaka uliopita hadi kufikia Sh64.52 trilioni kufikia Juni 30, 2021.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Machi 30, 2021 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2021 kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino.


Kichere amesema hivyo kuna ongezeko la Sh7.76 trilioni sawa na asilimia 13.7.


Hata hivyo, amesema kipimo cha deni la Serikali kinachotumia pato la Taifa, kinaonyesha deni hili bado himilivu.

Aidha, Kichere amesema miradi ya kujenga na kuboresha viwanja vya ndege 12 yenye thamani ya Sh1.02 trilioni iliyotekelezwa katika kipindi cha kati ya mwaka 2016/17 hadi 2020 2021 ilikaguliwa.


Amesema ukaguzi ulibaini kuwa kuna mwingiliano wa mamlaka na majukumu ya uendelezaji wa viwanja vya ndege mwingiliano Tanroad na TAA unaosababisha mapungufu na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi hiyo.


“Ukaguzi ulibaini kuna mwingiliano wa mamlaka na majukumu ya uendelezaji wa viwanja kati ya Tanroads (Wakala wa Barabara Nchini) na TAA (Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini) unaosababisha mapungufu ya uwajibikaji na utekelezaji wa bajeti,” amesema.


Pia Kichere amesema wamebaini kuna ongezeko la gharama ya Sh22.35 bilioni kutokana na kutolipa fidia kaya 1,125 katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa zaidi ya miaka 23.


Amesema kuna watu wanatakiwa kulipwa fidia lakini kuna taratibu hazijakamilika kwa hiyo tangu mwaka 1997 na kwamba tathmini inaonyesha deni linaongezeka kutoka Sh7bilioni na hivyo Sh29 bilioni.


Hali kadhalika CAG, amesema wamebaini ucheleweshaji wa malipo ya wakandarasi iliyosababisha tozo za riba ya Sh14.14 bilioni, ambapo Sh11.39 bilioni za Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere na Sh2.75bilioni za Kiwanja cha Ndege cha Mwanza.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu