Chelsea hali tete,Bilionea wake awekewa vikwazo ,timu yachukuliwa na serikali


Mmiliki wa klabu ya #Chelsea, Roman Abramovich amewekewa vikwazo na Serikali ya #Uingereza ikiwemo kuzuia Mali zake na marufuku ya kusafiri

-

Abramovich na Mabilionea wengine saba wamepata vikwazo hivyo baada ya kuonekana kuwa washirika wa Rais Vladimir Putin wa #Russia

-

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amesema haiwezi kuwa kimbilio salama kwa wanaounga mkono uvamizi wa Urusi kwa #Ukraine

Kufuatia vikwazo hivyo klabu ya Chelsea itaendeshwa chini ya leseni maalumu,ambapo bado haijawekwa wazi namna mshahaa utakavyokuwa ukilipwa kwa wafanyakkazi wa timu hiyo.

Sio jezi wala bidhaa nyingine za klabu hiyo ambazo zitauzwa kuanzia hivi sasa.


Hakutoongezwa mikataba kwa wachezaji wala usajili wa mchezaji yoyote kuja klabuni hapo.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu