CAG awakabidhi Takukuru ripoti za wapigajiWakati wadau mbalimbali hapa nchini wakitaka watumishi wa umma wanaohusika na ubadhirifu wawajibishwe, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema baadhi ya taarifa za ripoti za ukaguzi alioufanya zimechukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa ajili ya kuzifanyia kazi.


Pia, CAG Kichere ameshauri Sheria ya Manunuzi ya Umma ifanyiwe marekebisho ili kuondoa changamoto zinazojitokeza mara kwa mara na kusababisha fedha za umma kufujwa.


Kichere alibainisha hayo, katika mkutano uliowakutanisha watendaji wa ofisi ya CAG, wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na wanahabari wa vyombo vya habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam.


Alisema sheria ya manunuzi ya umma inatoa mwanya wa fedha za umma kufujwa na watendaji wasio waaminifu kupitia ununuzi wa vitu mbalimbali kupitia zabuni wanazozitangaza.


“Unakuta kitu sokoni kinauzwa Sh1,500 lakini watu wamenunua kwa Sh5,000 na unapofuatilia unaona wamekidhi matakwa na wamefuata sheria na taratibu zinazotakiwa...kuna haja ya kuifanyia marekebisho sheria ya ununuzi ili kunusuru fedha za umma,” alisema.


Alisema Kenya wameshafanya mabadiliko ya sheria kama hiyo, akisema ofisi ya CAG inajielekeza katika thamani halisi ya kitu kilichonunuliwa.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu