Bobi Wine atinga Baraza Kuu ChademaMwanasiasa wa upinzani na mwanamuziki maarufu nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amewasili katika ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Kuu la Chadema chenye ajenda saba ikiwemo kusikiliza rufaa ya wabunge wa Viti Maalumu 19.


Bobi Wine anahudhuria kikao hicho kama mgeni maalumu kinachofanyika leo Jumatano Mei 11, 2022 Dar es Salaam na kuhudhuriwa zaidi ya wajumbe 400 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.


Baada ya kuwasili Bobi Wine ambaye ni mpinzani mkubwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, alipokewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kisha kusalimiana na viongozi wa vyama vya upinzani akiwamo James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Hashim Rungwe (Chauma), Juma Duni Haji (ACT-Wazalendo) pamoja na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza.


Tayari viongozi wakuu wa Chadema na wajumbe wa Baraza Kuu wameshafika ukumbi kwa ajili ya kuanza kikao hicho chenje ajenda za taarifa ya kamati kuu, yatokanayo na kikao kilichopita, kupitia muhtasari wa kikao kilichopita na kuthibitisha ajenda.


Ajenda nyingine ni pamoja mikakati na mipango na bajeti ya uendeshaji wa chama ambapo ndani ya kuna mpango mkakati wa miaka mitano na mpango kazi wa 2022 na 2023 na bajeti sanjari na kuandaa ratiba ya uchaguzi mkuu wa ndani Chadema. Pia watajadili na kujaza nafasi za wajumbe wa bodi ya wadhamini ambazo zipo wazi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu