Besigye atoroka polisi nyumbani kwake, afika katikati mwa jiji na kuhutubia watuAliyekuwa mgombea wa urais nchini Uganda Dr. Kiiza Besigye, amekamatwa katikati mwa jiji la Kampala, baada ya kuwatoroka maafisa wa polisi ambao wamezingira nyumbani kwake kuhakikisha kwamba hatoki nyumbani.


Kulingana na vyombo vya habari vya Uganda, Besigye amekamatwa akiwa anahutubia watu katikati mwa jiji.

Mwanaharakati huo wa kisiasa amekuwa wakizuiliwa nyumbani kwake kwa zaidi ya wiki moja tangu alipoitisha maandamano y auma kupinga kuongezeka kwa bei ya bidhaa.

Akihutubia watu katikati mwa jiji la Kampala, Besigye amesema “tunastahili kujikomboa wenyewe. Hata hawa maafisa wa polisi wanastahili kujikomboa kwa sababu hata hawana chakula, hawana pa kulala.”

“Ni lazima bei za bidhaa zishuke, ni lazima wapunguze ushuru,” ameongezea Besigye.

Siku mbili zilizopita, rais wa Uganda Yoweri Museveni alihutubia taifa kwa zaidi ya saa mbili, na kusema kwamba utawala wake hautaingilia kati na kulazimisha bei ya bidhaa kushuka, akisema kwamba hatua hiyo inaweza kuangusha uchumi wa nchi.

Besigye alikuwa amejaribu kuondoka nyumbani kwake jana jumatatu lakini akakamatwa na kuzuiliwa kwa gari la polisi. Hadi wakati wa kuandaa ripoti hii, Besigye alikuwa anazuiliwa katika kituo cha polisi kikuu cha Kampla.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu