Bei ya mikate haishikiki Misr kisa vita ya Urusi na Ukraine,serikali yacharukaMisri imeweka ukomo wa bei ya mkate isiyowekewa ruzuku, katika kupambana na kasi ya kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu kutokana na mzozo wa vita kati ya Urusi na Ukraine.


Tangazo la ofisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo lililochapishwa na ofisi yake limesema bei ya kilo ya unga wa ngano itakuwa pauni 11.50 za Misri, ambazo ni sawa na senti 66 dola ya Marekani.


Bei ya chakula imekuwa ikiongezeka kutokana na kufungwa kwa njia ya Bahari nyeusi kufuatia kuzuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine, nchi mbili ambazo zinaongoza duniani kwa kuzalisha ngano.


Ukomo huo wa bei utadumu kwa muda wa miezi mitatu, na watakaoikiuka watakabiliwa na faini ya hadi pauni milioni tano za Misri. Mkate ni chakula kikuu kwa Wamisri wengi, ambacho bei yake ina athari za kisiasa.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu