Baraza kuu la umoja wa mataifa kuifukuza Urusi !!!Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo alhamisi litapiga kura kuhusu azimio lililowasilishwa na Marekani la kutaka Urusi isimamishwe uanachama katika baraza la haki za binadamu la Umoja huo.


Azimio hilo limependekezwa kufuatia tuhuma kwamba wanajeshi wa Urusi waliwauwa raia wakati wakiondoka kwenye eneo la karibu na mji mkuu wa Ukraine Kiev.


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield amesema wanaamini wanajeshi wa Urusi wametekeleza uhalifu wa kivita nchini Ukraine na wanaamini nchi hiyo inapaswa kubebeshwa dhamana.


Msemaji wa baraza kuu la Umoja huo wa Mataifa Paulina Kubiak amefahamisha kwamba kikao maalum kuhusu Ukraine kitafanyika leo na azimio hilo litapigiwa kura.


Baraza la haki za binadamu la Umoja huo makao makuu yake yako Geneva Uswisi na wanachama wake huchaguliwa kwa miaka mitatu na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu