Baada ya maandamano makubwa Rais Sudan akubali serikali ya mpitoKiongozi wa jeshi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema jeshi halitoshiriki mazungumzo ya kuukwamua mkwamo uliopo kati yake na upinzani wa kiraia.


Kama mbadala wa mazungumzo hayo yatakayoongozwa na jamii ya kimataifa, Al-Burhan ametoa wito kwa makundi ya kisiasa na mapinduzi kuanza mazungumzo ya kuunda serikali ya mpito.


Burhan ametoa tamko hilo katika televisheni wakati ambapo waandamanaji katika Mji Mkuu Khartoum wameongeza shinikizo kwa utawala wa kijeshi kwa kufanya maandamano yaliyodumu kwa siku kadhaa sasa kufuatia mauaji ya raia tisa Alhamis iliyopita wakati wa maandamano.


Mashuhuda wa shirika la habari la Reuters amesema karibu watu elfu 2 walikuwa wanashiriki maandamano hapo jana mchana. Tangu mapinduzi, makundi mengi ya kiraia yamekataa kufanya majadiliano na jeshi jambo lililopelekea mkwamo uliopo sasa.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu