Baada ya kupinduliwa na wananchi wake Rais Srilanka kukimbia nchiRais Gotabaya Rajapaksa aliyejiuzulu nchini Sri-Lanka amepelekwa katika kambi ya jeshi la wanaanga karibu na uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa hapo jana Jumatatu.


Hayo yameelezwa na maafisa nchini humo wakati zikiongezeka fununu kwamba ataikimbia nchi na kwenda uhamishoni ng'ambo.


Afisa mwandamizi katika wizara ya ulinzi amesema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 alikimbilia kwanza katika kambi ya jeshi la wanamaji kabla ya kupelekwa katika kambi ya jeshi la wanaanga ya Katunayake iliyoko karibu na uwanja mkuu wa ndege wa Sri-Lanka.


Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu aliko rais huyo ingawa vyombo mbali mbali vya habari nchini Sri-Lanka vimeripoti kuhusu tetesi kwamba anajiandaa kuelekea Dubai.


Kiongozi mkuu wa upinzani Sajith Premadasa kwa upande mwingine amesema wako tayari kuunda serikali.


Bunge litamchagua rais Julai 20. Pesa taslimu, rupee milioni 17.85 ambazo ni sawa na kiasi dola elfu 50 zilizoachwa na rais Rajapaksa katika makaazi yake zimekabidhiwa mahakama hii leo na waandamanaji.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu