Australia yatuma vifaru vya kijeshi kwa Ukraine yasema ni zawadiAustralia imetuma vifaru vya kijeshi 20 ilivyoipatia kama zawadi Ukraine, kufuatia ombi lililotolewa na rais wa Ukraine Zelensky wiki iliyopita.


Vifaru hivyo vizito vyinavyoweza kusafiri maeneo ya vichakani vitatumiwa kuwasafirisha wanajeshi na raia katika maeneo ya vita - havitatumuwa katika mashambulio ya vita.


Zelensky alitoa hotuba kwa njia ya video kwa bunge la Australia wili iliyopita – ikiwa taifa la 20 kulihutubia- alilishikuru taifa hilo kwa usaidizi wake thabiti kwa Ukraine.


Australia imeahidi kutoa dola milioni 190 za Australia (£108m; $142m) kwa ajili ya msaada wa kijeshi na kibinadamu na iliidhinisha vikwazo kadhaa dhidi ya raia binafsi wa Urusina uagizaji wa mafuta kutoka nchini humo.


"Bw Rais, watu wa Australia wako pamoja na Ukraine kwa ajili ya uwepo wake," alisema waziri mkuu wa Australia Scott Morrison alipokuwa akimjibu Bw Zelensky wiki iliyopita.


Kiongozi huyo wa Australiaamerutangaza mara kwa mara kwamba demokrasia huru lazima isimame pamoja kutetea uhuruna "haki ya kuishi kwa bila utangamano, vitisho na kulazimishwa kufanya mambo ".


Alisema Australia inamuheshimu Zelensky kama "simba wa demokrasia''

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu