Auawa kwa kumkumbatia mke wa mtu Njombe,alipigwa na tofali kichwaniMtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Razalius Kufabasi (50) mkazi wa kijiji cha Lusala wilayani Ludewa mkoani Njombe anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji ya Linus Mtega (52) kwa kumpiga na tofali usoni akimtuhumu kumkumbatia mkewe.


Imeelezwa kuwa siku ya tukio hilo kulikuwa na shughuli ya kujengea makaburi ambapo majira ya usiku watu walikuwa wakiburudika kwa muziki hivyo marehemu huyo alikuwa amemkumbatia mke wa mzee Kufabasi huku wakicheza pamoja kitu ambacho kilizua wivu kwa mzee huyo aliyeamua kuchukua tofali na kumpiga nalo mzee Mtega kwenye paji la uso.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mzee Mtega alichanika paji lake la uso ambapo alikimbizwa katika kituo cha afya cha Mlangali lakini hakuweza kupona na kufikiwa na umauti huku mtuhumiwa huyo akijaribu kutoroka lakini hakuweza kufanikiwa na kutiwa nguvuni na jeshi la polisi.


Aidha Kamanda Issa amelaani vikali tabia hizo huku akiitaka jamii kuacha wivu uliopitiliza kwani yanapotokea mauaji kama haya familia pamoja na watoto ndio huteseka.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu