Askari polisi ajiua kwa kujinyonga MbeyaJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limethibitisha kifo cha askari wake mwenye namba EX.SGI, Sajenti Novatus ambaye amejinyonga ndani ya nyumba yake eneo la Mwambene, Kata ya Mwakibete jijini Mbeya.


Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumatano Machi 16, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amesema Sajenti Novatus alikutwa amejinyonga jana mchana.


Amesema kuwa taarifa za awali zilieleza kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na kwamba haijafamika sababu ya kuchukua uamuzi huo wa kukatisha uhai wake.


''Hata sisi tunasikitika kwa askari wetu kukatisha uhai wake hivyo ningeomba kwa wakati huu tuwe watulivu kwani kifo chake ni kama vifo vingine''amesema.


Diwani Kata ya Mwakibete, Lucas Mwampiki amesema kuwa taarifa za awali kutoka kwa familia ya marehemu zinaeleza kuwa alikuwa likizo na jana mchana alirejea nyumbani akitokea kwenye matembezi na baada ya muda ikagundukika kajinyonga.


''Huyo bwana kwa taarifa nilizopata alikuwa likizo na baada ya kurejea nyumbani aliingia chumbani kwake na baada ya muda aligundulika akiwa amejinyonga na hivyo bado haijulikani sababu ya kujinyonga'' amesema

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu