Apoteza maisha kwa kula pipi zenye bangi ndani yakeMwanafunzi wa sheria nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 23, Damilola Grace Olakanmi, amefariki dunia baada ya kula pipi zenye bangi (gummy) huko London Mashariki.

Kituo cha habari cha Evening Standard kinasema, mwanafunzi huyo wa shahada ya kwanza ya sheria ya biashara katika Chuo Kikuu cha Hertfordshire alinunua pipi hizo kupitia programu ya ujumbe kwenye simu yake na zikaletwa nyumbani kwake.

Bi Olakanmi na rafiki yake mwenye umri wa miaka 21 walianza kujisikia vibaya mara tu walipotumia pipi hizowakiwa katika nyumba yao huko katikati mwa South Park Drive, IIford nchini Uingereza majira ya saa 11.30 jioni siku ya Jumanne, Machi 29 .

Bi Olakanmi alichukuliwa na ambulensi ya ndege hadi Hospitali ya Queen, Romford akiwa katika hali mbaya.

Mama yake Wumi, 51, anansema bini yake alifariki dunia Jumamosi, Aprili 2 baada ya jitihada zote za kuokoa uhai wake kugonga mwamba.

Mwanaume ambaye aliwaletea pipi hizo, Leon Brown, 37, wa Norwood Kusini, alikamatwa kuhusiana na tukio hilo siku ya Ijumaa.


Baadaye alishtakiwa kwa tuhuma za kusambaza bangi iliyoathiri akili na afya kwa ujumla ya binti huyo hadi kusababisha kifo.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu