Aliyemuua wziri mkuu Japan kuchunguzwa akiliMtu anayetuhumiwa kumuua waziri mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa hali yake ya kiakili ili kutathmini afya yake ya kiakili wakati wa tukio hilo.


Abe aliuawa kwa kupigwa risasi kwenye kampeni mnamo Julai 8 katika mji wa magharibi wa Nara, siku mbili kabla ya uchaguzi wa bunge nchini humo.


Mshukiwa wa muuaji hayo Tetsuya Yamagami mwenye umri wa miaka 41 yuko kizuizini na inasemekana alimlenga Abe kwa kuwa aliamini kiongozi huyo wa zamani alihusishwa na Kanisa la Muungano.


Mahakama ya Wilaya ya Nara iliidhinisha ombi la ofisi ya waendesha mashitaka la kufanyika uchunguzi wa kiakili unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.


Abe alikuwa mwanasiasa mashuhuri na maarufu zaidi nchini Japan, alijiuzulu mwaka 2020 kutokana na sababu za kiafya.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu