Alitaka kumuua waziri mkuu Hispania ,jela miaka 7Mahakama ya Hispania imemuhukumu kifungo cha miaka saba jela mwanaume aliyetishia kumuua waziri mkuu mwenye siasa za kisoshalisti, Pedro Sanchez, kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa jana Jumanne Aprili 12, 2022.


Manuel Murillo Sanchez, mlinzi wa usalama mwenye miaka 65 kutoka jiji la Terrassa lililo kaskazini mashariki, alikamatwa Septemba mwaka 2018 baada ya polisi kustushwa na ujumbe aliokuwa akituma kwenye kundi la WhatsApp la watu wenye siasa za mrengo wa kulia.


Aliwaambia wanakikundi hao kuwa anachukizwa na mipango ya waziri mkuu ya kufukua mwili wa dikteta Francisco Franco kutoka makaburi ya watu wa heshima karibu na Madrid, mpango ambao hatimaye ulitimizwa Oktoba mwaka 2019.


"Hatuwezi kuwaruhusu wamdhalilishe jenerali," aliandika katika ujumbe wake wa Aprili 11, kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa.

"Kama inahitajika nitaenda huko nikiwa na silaha na nitakaa juu ya kaburi la Franco na kama wakija, nitawafyatulia risasi."


Murillo Sanchez alieleza mara kadhaa nia yake ya kuondoa maisha ya waziri mkuu ili kufanya "mabadiliko katika hali ya kisiasa nchini Hispania", na kuomba msaada kutoka kwa wanakikundi kufanikisha mpango wake, hukumu hiyo inasema.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu