Akiri kukata viungo vya miili ya binadamu walioaga dunia na kuviuzaMwanamke Megan Hess amekiri mahakamani kuwa alikuwa akikata viungo vya miili ya binadamu walioaga dunia kisha kuiuza huko Colorado Marekani.


Mwanamke huyo aliyekuwa akisimamamia kampuni ya Sun set Mea inayojihusisha na kufanya mazishi ya binadamu kwa kuichoma miili ,ameiambia mahakama mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Marekani Gordon Gallagher huko Grand Junction, Colorado. siku ya jana Jumanne kuwa aliviuza viungo vya miili ya watu 12.


Viungo alivyodaiwa kuvikata na kuviuza ni pamoja na vichwa,mikono na miguu na kuviuza kwenye taasisi zinazofanya utafiti na mafunzo ya viuongo vya binadamu.


Kukiri huko kunakuja mara baada ya shirika la habari la Reauters kufichua mwaka 2018 juu ya biashara hiyo iliyokuwa ikifanywa na mwanamama huyo.


Hess, mwenye umri wa miaka 45, alikiri Jumanne kwamba kupitia nyumba yake ya mazishi, iliyoko katika mji wa Montrose katika sehemu ya magharibi ya jimbo hilo, alilaghai angalau familia kumi na mbili zinazotafuta huduma za kuchoma maiti kwa jamaa waliokufa.Hess alikuwa amepangiwa kuhukumiwa baada ya wiki tatu pamoja na mamake, Shirley Koch, ambaye hapo awali alikana mashtaka. Kesi ya mabadiliko ya rufaa ya Koch imepangwa Julai 12.


Baada ya Wakili Msaidizi wa Marekani Jeremy Chaffin kutoa pendekezo lake la hukumu, wakili wa Hess, Dan Shaffer, alihimiza kifungo chepesi cha takriban miaka miwili jela. Hess amekuwa huru kwa dhamana tangu kukamatwa kwake.


Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo, hakimu alimtaka Hess aeleze kwa maneno yake uhalifu aliofanya. Hapo awali Hess aliita suala zima "uharibifu wa kisheria." Alipotakiwa na hakimu kujieleza kujieleza, Hess alikubaliana na upande wa mashtaka aliwalaghai wahasiriwa wake, ingawa alikataa kuelezea kwa undani.Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu