Ajali ya Tanga ni Hiace iligonga gari mbovuMkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima ametembelea eneo kulikotokea ajali jana usiku Wilayani Handeni mkoani Tanga na kuua Watu wanne.


RC Malima amezungumza na baadhi ya walioshuhudia ajali hiyo ambao wamemueleza kwamba ilitokea baada ya Toyota Coaster ikiwa na abiria ikitokea Korogwe kuelekea Handeni kugonga baadhi ya Wananchi waliokuwa wakisaidia kuziba pancha kwenye hiace iyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara.


"Hiace ilikuwa imepasuka tairi na kulikuwa na Wanakijiji wanasaidia kubadilisha tairi, wakati coaster inakuja akawa anaelekezwa asimame lakini kwasababu haikuwa na taa ikagonga wale wanakijiji waliokuwa wanasaidia na kuanguka huko bondeni, kwa hiyo waliopata ajali wengi ni Wananchi” shuhuda


RC ameongozana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo ambapo Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni wakiendelea na matibabu.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu