Ajali: watu 18 wafariki kwa ajali ya Basi IringaWatu 18 wamefariki dunia papo hapo baada ya basi dogo aina ya Costa kugongana uso kwa uso na lori la mizigo karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkiani Iringa.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amethibitisha kutokea vifo hivyo akisema kuwa taarifa ziaidi zitatolewa baadaye.


"Ni kweli ajali imetokea na inasadikika watu zaidi 10 wamepoteza maisha papo hapo," amesema.


Wakizungumza kwa njia ya simu baadhi ya watu walio katika eneo la tukio wamesema mpaka saa tatu asubuhi, jitihada za kuokoa majeruhi na kutoa miili ya watu zinaendelea.


Eneo ambalo ajali hiyo imetokea, ndilo ambalo basi la Majinja liliangukiwa na lori mwaka 2015 na kuua zaidi ya watu 40.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu