Ajabu: Polisi wakaa kikao na wafanyabiashara za ngono,sasa kuwatumia kuimarisha usalamaPolisi nchini Malawi wamekaa na wanawake wafanyabiashara za ngono kwa lengo la usikiliza kero zao na pia kushirikiana nao katika masuala ya kiusalama.


Picha zimesambaa zikiwaonesha polisi wa eneo la Kawale katika mji mkuu wa taifa hilo wa Lilongwe wakiwa pamoja na wanawake hao wakijadiliana namna bora ya kushirikiana.


Kikao hicho kimefanyika Machi 16, 2022 ambapo Inspekta wa polisi Grace Vindevu amesema mkutano huo umeuwa na tija na kuwafumbua macho baadhi ya matukio ya uhalifu ambayo wanawake hao huyaona.


Akiwakilisha kundi hilo, mmoja wa wafanyabiashara ya ngono alitoa shukrani kwa polisi hao kwa kuwashirikisha katika masuala ya usalama.


Pia alitumia mkutano huo kama fursa ya kueleza baadhi ya matatizo wanayokumbana nayo wakati wa kuwahudumia wateja wao huku akitolea mfano unyanyasaji kutoka kwa baadhi ya wateja na wengine kushindwa kuwalipa baada ya kutoa huduma akisema hivyo ni kurudisha nyuma biashara zao.


Biashara a ngono ni haramu katika nchimbalimbali hasa za Afrika kutokana na hatari mbalimbali ikiwemo za kiafya kwa uwa isababishi cha magonjwa ya zinaa na hata ukimwi,kudhalilisha utu wa mwanamke na pia kuwaweka katika kila hatari zikiwemo za kuuawa na watu wasiojulikana.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu