28 wauawa Sudan kusini katika jaribio la wizi wa mifugoWatu 28 wameuawa wakati wa jaribio la wizi wa mifugo nchini Sudan Kusini. Mashambulizi hayo yametokea katika eneo la Leer la jimbo la kaskazini la Unity.


Kamishna wa kaunti ya Leer Stephen Taker amesema washambuliaji walikuwa ni vijana kutoka kaunti jirani za Mayendit na Koch.


Kamishna huyo amesema wavamizi 18 walifariki. Watu 10 wa Leer walikufa katika shambulizi hilo, wakiwemo wachungaji vijana na mwanamke mmoja.


Kaunti ya Leer iliathirika pakubwa na mgogoro wa kibinaadamu ambao ulizuka kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kati ya mwaka wa 2013 na 2018.


Vita hivyo viliuwauwa karibu watu 400,000 na kuwaacha mamilioni ya wengine bila makaazi. Karibu raia 72 waliuawa kati ya Februari 17 na Aprili 7 katika kaunti ya Leer kutokana na machafuko ya kikabila.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu