Marekani yakataa kuwasilisha ushahidi wa kuhusika Saudia katika tukio la Septemba 11 kwa familia za


Serikali ya Marekani kwa kisingizio cha usiri wa baadhi ya nyaraka za tukio la Septemba 11, 2001 imekataa kuziwasilisha nyaraka hizo kwa familia za wahanga wa tukio hilo.

Gazeti la Independent liliandika jana Alhamisi kuwa, William Barr, Waziri wa Sheria wa Marekani na Richard Grenell, Kaimu Mkuu wa Kituo cha Usalama wa Taifa nchini Marekani na kwa kisingizio cha 'masuala ya usalama wa taifa' wamesema kuwa, hawatozikabidhi familia za wahanga nyaraka zinazohusiana na kuhusika Saudi Arabia katika shambulio la Septemba 11 2001.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, katika vikao vya kuchunguza faili la Septemba 11 katika moja ya mahakama za Marekani wiki hii, William Barr na Richard Grenell walitoa madai mapya kwamba, nyaraka zinazoihusisha serikali ya Saudia katika tukio hilo,

kwa kuwa zinahesabika kuwa sehemu ya nyaraka za siri na kwa lengo la kulinda usalama wa taifa, zinatakiwa kuendelea kubakia kuwa za siri.

Kutopatiwa familia za wahanga wa tukio la Septemba 11, 2001 nyaraka hizo, kunapunguza fursa yao ya kuweza kuiburuza serikali ya Riyadh mahakamani kama zilivyokuwa zimepanga.

Katika uwanja huo, miezi kadhaa iliyopita gazeti la New York Times lilifichua kuwepo njama ya serikali ya Marekani ya kuiepusha Saudia na uhusika wake katika mashambulizi ya Septemba 11, 2001.

Uhusiano mkubwa uliopo kati ya Washington na Riyadh ndio sababu ya Saudia kutoburuzwa mahakamani kutokana na ugaidi wake

Katika tukio hilo, ndege nne za abiria zilitekwa nyara kwa lengo la kushambulia maeneo muhimu ya Marekani.

Ndege mbili na katika kipindi kilicho chini ya dakika 20 zilishambulia minara pacha ya Shirika la Biashara Duniani mjini New York,

huku ndege moja nyingine ikilenga jengo la Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon.)

Aidha ndege ya nne ilianguka katika eneo la mji wa Shanksville,

katika tukio ambalo hadi sasa bado halifahamika chanzo chake. Katika mashambulizi hayo kwa akali watu 3000 walipoteza maisha.

Watu 15 kati ya 19 waliohusika na shambulizi hilo la Septemba 11, walikuwa raia wa Saudi Arabia huku watu wawili wengine wakiwa ni raia wa Imarati.

Hata hivyo serikali tofauti za Marekani na kutokana na uhusiano mkubwa zilizonao na Saudia na pia kutokana na mikataba mingi ya kijeshi ya mabilioni ya dola iliyotiwa saini na pande mbili, zimekuwa kizuizi cha kushtakiwa Riyadh kuhusiana na faili hilo.

Idolojia ya kuchupa mipaka ya Uwahabi inayofundishwa nchini Saudia na kuungwa mkono na utawala wa Aal-Saud, ndilo chimbuko la ugaidi unaochochea jinai zinazotekelezwa katika pembe tofauti za dunia.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu