Shirika la Ujasusi la Israel MOSSAD lakiri kupora maski na vifaa vya tiba

April 17, 2020

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Shirika la Ujasusi la Israel MOSSAD amekiri juu ya kuibwa na shirika hilo maski na vifaa vya afya kwa lengo la kukabiliana na mgogoro wa virusi vya Corona ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (yaani Israel.)

 

Hayo yamesemwa na mkuu wa kituo cha teknolojia cha MOSSAD katika mahojiano na moja ya kanali za satalaiti za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kuhusiana na namna ya kukabiliana na mgogoro wa virusi hatari ya Corona ndani ya Israel.

 

Amesema kuwa katika kudhamini maski na vifaa vya afya kwa ajili ya utawala haramu wa Israel, Shirika la Ujasusi la Israel limekuwa likipora vifaa hivyo baada ya nchi nyingi duniani kukataa kuuza bidhaa hizo kutokana na kukumbwa na ugonjwa wa Covid-19.

 

Katika uwanja huo, gazeti la New York Times la nchini Marekani limeelezea nafasi ya shirika hilo katika kuiba taarifa za intelejensia, vifaa, nyenzo za tiba na za uangalizi wa wagonjwa kutoka nchi tofauti za dunia katika kipindi hiki cha kuenea virusi vya Corona.

 

Utawala bandia wa Kizayuni uliopora ardhi za Wapalestina, unapora mali za watu ili kujikinga na Corona

 

Gazeti hilo limefafanua kuwa, maafisa wa Shirika la Ujasusi la Israel MOSSAD wamejikita katika shughuli za afya ya jamii na kupora vifaa vya afya kimataifa.

 

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, ili kufanikisha wizi wa vifaa hivyo vya matibabu, shirika hilo la utawala bandia wa Kizayuni limeanzisha idara kubwa ya operesheni za uporaji.

 

Aidha serikali ya Israel imelitaka shirika hilo kuandaa zaidi ya vifaa milioni 130 vya tiba na dawa za kukabiliana na virusi vya Corona katika ardhi hizo za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

 

Hadi sasa watu elfu 12, 855 wameathirika na virusi vya Corona ndani ya Israel.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon