Magaidi 27 waliopewa mafunzo na Marekani wajisalimisha kwa jeshi la Syria


Mkuu wa kituo cha upatanishi baina ya pande hasimu nchini Syria kiichoko chini ya Wizara ya Ulinzi wa Russia amesema kuwa, magaidi 27 ambao wamepewa mafunzo na Marekani kwa ajili ya kushambulia taasisi za mafuta na miundombinu nchini Syria, wamejisalimisha kwa jeshi la serikali.

Shirika la habari la Sputnik la Russia limemnukuu Oleg Goravlov akitangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, baada ya kujisalimisha kwa jeshi la Syria magaidi wote hao wamekiri kwamba walipewa mafunzo na Marekani kwa ajili ya kushambulia taasisi za mafuta na gesi pamoja na taasisi za uchukuzi ndani ya Sryia. Mafunzo mengine waliyopewa na magaidi wa Kimarekani ni namna ya kuyafikishia silaha magenge ya kigaidi nchini Syria.

Ameongeza kuwa, kundi hilo lilishambuliwa na magaidi wengine wanaojiita Jaish al Maghawir. Walipoteza malori matatu katika mapigano lakini magaidi 27 kati yao walifanikiwa kutoroka na kukimbilia upande wa wanajeshi wa Syria. Sasa hivi magaidi hao 27 wako chini ya ulinzi wa wanajeshi wa Syria huko Tadmur.

Mwananchi wa Syria akiipiga kwa mawe gari ya wanajeshi vamizi wa Marekani

Ameongeza kuwa, magaidi hao waliojisalimisha kwa jeshi la Syria, wamelipa jeshi hilo la serikali makumi ya silaha nyepesi na za wastani ambazo baadhi yake zimetengenezwa na nchi za Magharibi.

Baada ya tukio hilo, tume ya kuratibu masuala ya Syria na Russia imetoa tamko na kuishutumu vikali Marekani kwa kutumia chaka la misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi, ili kuyapelekea silaha magenge ya kigaidi.

Hadi hivi sasa watu milioni 12 kati ya jamii ya watu milioni 23 na laki tano wa Syria wamekuwa wakimbizi. Kati ya hao milioni 12, milioni sita na laki tano wamekimbilia nje ya Syria na karibu milioni 5 na laki tano wamekimbilia maeneo mengine ndani ya Syria kwenyewe.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu