Mashirika ya UN: Huenda watoto milioni 117 wakakosa chanjo ya surua kutokana na COVID-19


Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa yanayohusika na afya yametahadharisha kuwa, watoto zaidi ya milioni 117 wanaweza kukosa chanjo ya kinga ya surua kutokana na janga la dunia nzima la COVID-19 linavyolazimisha watu kukaliana mbali kimwili na kijamii na kuathiri pia utoaji huduma za afya.

Taarifa iliyotolewa na shirika la Uanzishaji Juhudi la Surua na Rubella (M&RI), linalopewa msukumo na Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na mashirika mengineyo imeeleza kuwa, kampeni za utoaji chanjo ya kinga ya surua zimesha ahirishwa katika nchi 24, huku idadi ya nchi hizo ikitarajiwa kuongezeka na kuwafanya watoto katika nchi 37 duniani wawe hatarini kukumbwa na ugonjwa huo.

Shirika hilo linawahimiza viongozi husika kufanya juhudi za kuwafuatilia watoto waliokosa chanjo ili kuhakikisha wale walio hatarini zaidi kupatwa na ugonjwa wa surua wanadungwa chanjo ya ugonjwa huo haraka, mara tu itapowezekana kufanya hivyo.

Wakati ugonjwa wa matatizo ya kupumua wa COVID-19 tayari umeshaua zaidi ya watu 113,000 duniani kote hadi sasa, hofu ya mripuko wa surua ni tishio jingine linalotishia afya, hasa za watoto ulimwenguni.

Mwezi Desemba mwaka jana, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa, mnamo mwaka 2018 ugonjwa wa surua uliwakumba karibu watu milioni 10 duniani na kuua 140,000, akthari yao wakiwa ni watoto, katika kile lilichokielezea kama hali ya "kutisha.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu