Rais Erdoğan akataa ombi la kujiuzulu Waziri wake wa Mambo ya Ndani

April 13, 2020

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki ametupilia mbali ombi la kujiuzulu Waziri wake wa Mambo ya Ndani.

 

Kufuatia ukosoaji mkali kwa Süleyman Soylu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki kutokana na msongamano katika baadhi ya miji ya Uturuki, hasa baada ya kutangazwa amri ya kutotoka nje ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona, jana Jumapili alitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo. Pamoja na hayo asubuhi ya leo vyombo vya habari nchini humo vimetangaza kuwa, Rais Recep Tayyip Erdoğan amekataa kujiuzulu Süleyman Soylu na kumtaka aendelee kubakia katika nafasi hiyo.

Virusi vya Corona, changamoto kuu ya duniani

 

Amri ya kutotoka nje nchini Uturuki ilitangazwa Ijumaa usiku, hata hivyo muda punde kabla ya kutekelezwa kwake, wakazi wa baadhi ya miji ya nchi hiyo ukiwemo mji wa Istanbul, walivamia maduka kwa lengo la kununua vyakula na vinywaji.

 

Kufuatia hali hiyo, serikali ya Ankara ililazimika kufuta amri hiyo. Kama ombi la kujiuzulu Süleyman Soylu lingekubaliwa, basi angekuwa waziri wa pili kujiondoa katika serikali ya Erdoğan baada ya kutangazwa kuenea virusi vya Corona nchini Uturuki. Wiki mbili zilizopita, Waziri wa Usafirishaji wa nchi hiyo alijiuzulu wadhifa wake. Hadi Jumapili ya jana idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona nchini Uturuki ilikuwa 1198.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon