Gharama kubwa za safari za familia ya Trump zaathiri wananchi wa Marekani

April 13, 2020

Duru za habari zimefichua utumiaji mkubwa wa siri wa vyombo vya usalama vya Marekani kwa lengo kuwasindikiza watu wa familia ya Trump katika safari zao.

 

Gazeti la Daily Mail linalochapishwa kwa lugha ya Kingereza limeripoti kuwa watu wa familia ya Trump mbali na Rais mwenyewe wa nchi na mkewe Melania wamefanya safari 4000 katika kipindi cha miaka mitatu ya fedha ya urais wa Trump huku wakilindwa na vyombo vya usalama vya siri. 

 

Daily Mail limeandika kuwa kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Fedha ya Marekani, safari hizo ni mara tatu ya zile zilizofanywa mwaka 2010 hadi 2016 na familia ya Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama. 

 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa safari kadhaa za familia ya Trump ambazo zilifanyika chini ya ulinzi wa vyombo vya usalama vya siri  katika mwaka uliopita wa fedha zinazidi safari zote za familia ya Obama katika kipindi cha miaka saba. 

Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama na familia yake 

Taarifa ya Wizara ya Fedha ya Marekani imeongeza kuwa familia ya Obama kila mwaka ilifanya jumla ya safari 133 kwa kupatiwa ulinzi huku familia ya Trump ikitajwa kwa wastani  kwa mwaka kufanya safari zipatazo 1625 chini ya ulinzi wa siri.   

 

Wakati huo huo gazeti la USA Today limeripoti kuhusu suala hilo kwamba gharama za vyombo vya usalama vya siri katika safari za wana wawili wa kiume wakubwa wa Trump ziligharimu kiasi cha dola 230,000 kila mwezi katika mwaka juzi wa 2018.

 

Rais wa Marekani alichukua uamuzi wa kuwakabidhi wanawe hao wakubwa wa kiume uendeshaji wa masuala yake ya biashara baada ya wataalamu na wawakilishi wa kongresi ya nchi hiyo mwezi Januari mwaka 2018 kubainisha wasiwasi wao kuhusu shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Trump.

 

www.mzunguko.com       

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon