Sudan yaadhimisha mwaka mmoja wa mapinduzi dhidi ya Bashir

April 11, 2020

Ni mwaka wa kwanza wa Sudan tangu kuondolewa kwa dikteta Omar al-Bashir. Lakini hakuna cha  kusherehekea. Uchumi bado uko dhaifu, hali ya kisiasa bado ni tete, wakati janga  la COVID-19 linazusha mtafaruku mwingine.

Mwaka mmoja  uliopita , mamia  kwa  maelfu ya  raia  wa  Sudan  walifanya maandamano  ya wiki  nzima mbele ya  makao makuu  ya  jeshi  katika  mji mkuu  wa  nchi  hiyo  Khartoum.

 

Mwanafunzi kijana  mwanamke , Alla Salah , alisimama  juu  ya  kipaa  cha  gari  akiimba kauli mbiu za kisiasa, baadaye  alikuja  kuwa  ishara  ya  vuguvugu la maandamano  katika jamii  ambayo  kwa  kiasi  kikubwa  inadhibitiwa  na  wanaume zaidi.

Kiongozi wa maandamano nchini Sudan Ahmed Rabie akionesha ishara ya ushindi pamoja na jenerali wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan

 

Kila  mmoja  aliingia  mitaani, ikiwa  ni  pamoja  na  maprofesa, waalimu  na  madaktari. Wasanii waliandika  ujumbe  na kuchora   picha za  uhuru katika  kuta mjini  Khartoum.

Kwa miezi  kadhaa , nchi  hiyo  ilikuwa  ikitokota  hadi  hatimaye  kile  ambacho hakikufikirika  kikatokea: dikteta  Omar al-Bashir alipinduliwa  Aprili 11, 2019, baada  ya karibu miongo mitatu  madarakani.

 

Yalikuwa  mapinduzi  yaliyoelezwa  na  wengi  kuwa  ni vuguvugu  la  mapinduzi ya  mataifa ya  Kiarabu namba  mbili. Raia walijisikia  furaha  kubwa.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon