Mgogoro wa corona barani Ulaya, zaidi ya nusu ya vifo vyote duniani vimetokea katika nchi tano kubwa za bara hilo

April 11, 2020

Ugonjwa wa COVID-19 umeendelea kuwa tishio kubwa duniani huku Marekani na nchi za Ulaya zikiwa kitovu cha maambukizi ya kirusi cha corona. Idadi ya vifo na maambukizi imeongezeka sana Marekani na barani Ulaya.

 

Huku idadi ya maambukizi na vifo ikiongezeka sana nchini Marekani, jana usiku serikali ya Italia ilitangaza kuwa, watu wengine 3,951 wamethibitika kukumbwa na ugonjwa wa COVID-19 katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na kufanya idadi ya walioambukizwa corona nchini humo kufikia watu 147,577 huku hadi kufikia jana watu 18,849 walikuwa wameshafariki dunia kwa ugonjwa huo  huko Italia. 

 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya serikali, nchi hiyo ya Ulaya ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu waliopoteza maisha kwa corona duniani ikifuatiwa na Marekani ambayo imetangaza watu 18,747 waliofariki dunia kwa ugonjwa huo hadi jana Ijumaa. 

 

Maambukizi ya corona mjini London, Uongereza

 

Hata hivyo Marekani ndiyo inayoongoza kwa mbali kati ya nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa corona duniani. Hadi jana Ijumaa, zaidi ya nusu milioni ya watu walikuwa wameshathibitishwa kukumbwa na corona nchini Marekani. 

 

Nchi nyingine zenye idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya corona barani Ulaya ni Uhispania, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. Hadi wakati tunaandika habari hii, watu 59,821 walikuwa wameripotiwa kufariki dunia katika nchi hizo tano kuu za Ulaya, hiyo ikiwa ni zaidi ya nusu ya watu wote waliofariki dunia kwa ugonjwa huo kote ulimwenguni. 

 

Ugonjwa wa Covid-19 uligunduliwa kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan, China mwisho mwa mwaka uliopita wa 2019. Hadi hivi sasa ugonjwa huo umeshaenea kote ulimwenguni. Zaidi ya watu  Laki moja na 2,734 (102,734) wameshafariki dunia kwa ugonjwa huo kote ulimwenguni. 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon