Idadi ya wahanga wa corona nchini Marekani yapindukia elfu 16, jana pekee iliua karibu elfu mbili

April 10, 2020

Maiti za wahanga wa corona, Marekani

 

 

Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti jana usiku kwamba idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini humo imepindukia 468,566 na kwamba 16,691 miongoni mwao wameaga dunia kutokana na virusi hivyo. 

 

Jana peke yake Wamarekani karibu elfu mbili waliaga dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona ambavyo sasa vinaelekea kulemaza uchumi wa nchi hiyo.  

 

Marekani inaongoza dunia katika orodha ya nchi zote zilizopatwa na mlipuko wa virusi vya corona.

 

 

Marekani ilichukua hatua ya kushughulikia wagonjwa wa corona kwa kuchelewa na sasa inasumbuliwa na uhaba wa vifaa vya kupima virusi hivyo na zana za kitiba za waathirika wa corona. Sasa nchi hiyo inatajwa kuwa ndiyo kitovu kikuu cha maambukizi ya corona kuelekea maeneo mengine ya dunia. 

 

Siku chache zilizopita Mkuu wa Afya wa Serikali ya Federali ya Marekani amesema wiki hii itakuwa "ngumu na ya kusikitisha zaidi" kwa "maisha ya Wamarekani wengi," na amekielezea kipindi kibaya kijacho cha janga la virus vya corona nchini humo kuwa kitakuwa sawa na kile cha "wakati wa mashambulizi ya Pearl Harbor" na "11 Septemba mwaka 2001."

 

Corona inaendelea kuchukua roho za maelfu ya Wamarekani

 

Vilevile wataalamu wa White House wametabiri kuwa Wamarekani baina ya laki moja na laki mbili na arubaini elfu watapoteza maisha kutokana na maambukizi ya virusi ya corona. 

 

Utendaji mbaya wa serikali na haba wa vifaa na zana za tiba nchini Marekani umeendelea kukosolewa sana na wanasiasa na wananchi wa nchi hiyo, suala ambalo wachambuzi wa mambo wanasema litakuwa na taathira kubwa katika matokeo ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon