Corona yawapata wanamfalme 150 wa Saudi Arabia akiwemo Gavana wa Riyadh, Faisal bin Bandar

April 10, 2020

Gavana wa Riyadh , Faisal bin Bandar bin Abdulaziz Aal Saud amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

 

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa virusi vya corona vimeshambulia kwa kiwango kikubwa famia ya kifalme ya Saudi Arabia.

 

 

Gazeti la New York Times la Marekani limefichua kuwa, karibu wanamfalme 150 wa ukoo wa Aal Saud unaotawala Saudi Arabia wameambukizwa virusi vya corona. 

 

Likiwanukuu watu wa karibu la utawala wa Saudia, gazeti hilo limefichua kuwa, virusi vya corona vimewasibu baadhi ya wanamfalme wenye vyeo na nafasi za juu katika utawala wa kifalme wa Saudia. 

 

Ripoti hiyo inasema miongoni mwa wanamfalme waliopatwa na virusi vya corona ni pamoja na Gavana wa Riyadh, Faisal bin Bandar bin Abdulaziz Aal Saud ambaye amehamishiwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi.

 

Kuna maelfu ya wanamfalme nchini Saudi na wengi wao husafiri kwenda Ulaya mara kwa mara na inasadikiwa kuwa wamepata virusi hivyo nje ya nchi na kuirudi navyo Saudi Arabia.

 

Ripoti hiyo pia imesema kuwa Mfalme Salman bin Abdulazizi wa Saudi Arabia amehamia katika kasri iliyoko kwenye kisiwa kidogo katika Bahari Nyekundu karibu na mji wa Jiddah kwa hofu ya kuambukizwa virusi vya corona.

Mfalme Salman bin Abdulazizi wa Saudi Arabia

 

Waziri wa Afya wa Saudi Arabia, Tawfiq al Rabiah amesema kuwa wanajiandaa kwa kesi laki mbili na maambukizi ya virusi vya corona.    

 

Hadi sasa watu 3,122 wameambukizwa virusi vya corona nchini Saudi Arabia na makumi miongoni mwao wameaga dunia kutokana na gonjwa huo.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa virusi vya corona vimeshambulia kwa kiwango kikubwa famia ya kifalme ya Saudi Arabia.

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon