Idadi ya wahanga wa corona huko New York ni zaidi ya wale wa mashambulio ya Septemba 11

April 9, 2020

Idadi ya watu walioaga dunia kwa maambukizi ya virusi vya corona katika mji wa New York nchini Marekani ni zaidi ya wale waliofariki dunia katika mashambulizi ya Septemba 11 katika kituo cha kimataifa cha biashara mjini humo.

 

Gazeti la The Boston Globe linalochapishwa nchini Marekani limeandika kuwa maafisa wa tiba wa Marekani wametangaza kuwa kwa uchache watu 3,250 wameaga dunia huko New York kufuatia kuambukizwa virusi vya corona.

 

Aidha watu 2,753 waliuliwa katika mashambulio hayo ya Septemba11 ambayo yanatajwa kuwa ya maafa makubwa zaidi ya roho kufanywa ndani ya ardhi ya Marekani.  

 

Andrew Cuomo, Gavana wa jimbo la New York jana alitangaza kuwa wamesajili kesi mpya 731 za watu walioaga dunia kwa kuambukizwa virusi vya corona jimboni humo. Amesema idadi ya watu walioaga dunia kwa maambukizo ya corona huko New York imefikia karibu 5,500. 

 

Gavana wa New York, Andrew Cuomo  

 

Marekani inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya corona. Hadi sasa watu laki nne na 412 wamepatwa na maambukizi ya corona nchini humo na wengine 12,854 wameaga dunia. 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon