Israel yakumbwa na mgogoro mkubwa katika sekta ya afya


Kuenea virusi vya Corona katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kushindwa utawala haramu wa Kizayuni katika kuzuia maambukizi ya maradhi hayo, kumepelekea kushtadi wasi wasi mkubwa baina ya viongozi wa utawala huo.

Gazeti Haaretz la utawala huo limenukuu taarifa ya kitengo cha uangalizi cha Wizara ya Afya ya Israel ikielezea uwepo wa takwimu kinzani katika siku za hivi karibuni kuhusiana na maabara za Israel. Akielezea suala hilo Morris Dorfman, mkuu wa kitengo cha uangalizi cha Wizara ya Afya ya Israel amesema kuwa, kutokana na takwimu kinzani, imeamuliwa kufanyika uchunguzi wa maabara zote ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Benjamin Netanyahu

Sambamba na kutuma taarifa kwenda kwa viongozi wa utawala wa Kizayuni, Dorfman amesisitiza kuwa, iwapo virusi vya Corona vitaenea na kuikumba robo moja ya Wazayuni, basi Wizara ya Afya ya Israel haitokuwa tena na uwezo wa kukabiliana na mgogoro huo.

Katika taarifa hiyo inatarajiwa kuwa iwapo maambukizi ya virusi vya Corona yataendelea kama ilivyo sasa, hospitali za Israel zitakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa tiba, vitanda na madawa. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni, idadi ya waathirika wa virusi vya Corona ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu imefikia elfu 6 na 92 pamoja na watu 28 waliofariki dunia.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu