Serikali za Afrika kushirikiana na makampuni ya teknolojia kukabiliana na taarifa za uwongo kuhusu corona

April 3, 2020

Serikali za nchi barani Afrika zinashirikiana na makampuni ya teknolojia kama Facebook na WhatsApp ili kukabiliana na upotoshaji wa taarifa kuhusu virusi vya corona katika mitandao ya kijamii ambao unaweza kuzidisha maambukizi ya virusi hivyo katika bara hilo lenye mifumo ya afya inayolegalega. 

 

 

Afrika Kusini ambayo ina maambukizi zaidi ya virusi vya corona kuliko nchi nyingine barani Afrika ikiwa tayari imethibitisha kuwa na kesi 1,300, imeanzisha kitengo cha huduma ya habari kuhusu virusi vya corona katika mtandao wa WhatsApp.

 

Nchini Nigeria maafisa wa Afya hivi sasa wanachangia huduma ya habari inayomilikiwa na Facebook kutuma taarifa kwa watumiaji zinazotoa ushauri kuhusu dalili na namna ya kujiepusha na maambukizi ya corona.

 

Kitengo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Nigeria NCDC pia kinanufaika na huduma ya bure ya nyongeza katika mtandao wa Facebook ili kusambaza taarifa kuhusu maambukizi ya virusi vya corona.

 

Huduma hii pia imetolewa kwa nchi nyingine 11 za Kiafrika na katika sehemu nyingine duniani. 

Wahudumu wa Afya, Afrika Kusini

 

Mkuu wa Kitengo hicho cha Nigeria cha Kudhibiti Magonjwa, Chikwe Ihekweazu amesema kuwa hawajawahi kuwa na wakati mgumu kama hivi sasa ambapo wamelazimika kutegemea pakubwa mitandao ya kijamii kutuma taarifa zilizo sahihi.

 

Hata hivyo srikali na makampuni ya teknolojia hivi sasa yanakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na taarifa za uongo zinazosambazwa kupitia majukwaa mbalimbali huku maambukizi ya virusi vya corona yakizidi kuongezeka.

 

Ametolea mfano wa baadhi ya ujumbe wa Twitter uliotumwa na mtumiaji mmoja kutoka Kenya ambaye ana wafuasi karibu laki saba usemao: 

 

"Watu weusi hawapati maambukizi ya corona”.  Amesema baadhi ya serikali zimeanza kuwachukulia hatua watu wanaotuma jumbe za namna hii.

 

Kenya imewatia mbaroni wanaume wawili akiwemo bloga mtajika kwa kosa la kusambaza taarifa za uwongo kuhusu corona kupitia Twitter. Kosa hilo linagharimu kifungo cha jela cha hadi miaka kumi au faini ya shilingi milioni tano za Kenya ambazo ni sawa dola za Kimarekani 48,000.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon