Kenya, Somalia zawaachilia huru wafungwa ili kuzuia kuenea corona

April 3, 2020

Kenya na Somalia zimetangaza kuwaachilia huru wafungwa wa makosa madogo madogo ikiwa ni katika jitihada za kupunguza msongamano katika magereza katika kipindi hiki cha kuenea ugonjwa hatari wa corona au COVID-19.

 

Siku ya  Alhamisi Kenya ilitangaza kuwaachilia huru wafungwa  3,837 ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 katika magereza. Taaarifa ya Idara ya Magereza Kenya imesema uamuzi huu unalenga kuhakikisha kuwa kila mtu anakaa umbali wa mita moja na mwenzake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kimataifa katika vita dhidi ya janga la COVID-19.

Aidha Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga ameamuru kuwa wanaofanya makossa madogo madogo na makossa ya trafiki wasikae katika seli za vituo vya polisi kwa zaidi ya masaa 24.  Kwa upande wake, Rais wa Somalia ametoa msamaha kwa wafungwa 148 ikiwa ni juhudi za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona

 

Rais Mohamed Farmajo wa Somalia, ametoa msamaha kwa wafungwa 148 ikiwa ni sehemu ya hatua za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona nchini humo

 

Rais huyo amesema, kuachiwa kwa wafungwa hao waliofanya makosa madogo kunafuatia ripoti iliyowasilishwa kwake na mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu hali ya wafungwa nchini humo wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.

 

Pia Rais Farmajo amezielekeza mamlaka za magereza na wizara ya afya kuchukua hatua mwafaka kuzuia mgogoro wa kiafya kwa wafungwa waliobaki gerezani.

Mpaka sasa, kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini Somalia zimefikia tano, zikiwa ni raia watatu wa Somalia na raia wawili wa kigeni.

 

Hadi sasa watu 110 wameambukizwa corona nchini Kenya na miongoni mwao watatu wamefariki huku katika nchi jirani ya Somalia walioambukizwa wakiwa ni watano.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon