Jumuiya tatu za UN zatahadharisha kuhusu hatari ya baa la njaa duniani

April 2, 2020

Wakuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Biashara Duniani (WTO) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wametahadharisha kuwa, iwapo nchi mbalimbali zitashindwa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, dunia itakumbana na hatari ya uhaba wa chakula.

 

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Qu Dongyu, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom na Mkurugenzi Mkuu wa WTO, Roberto Azevêdo wametoa taarifa ya pamoja wakisisitiza kuwa, maambukizi ya virusi vya corona yamesababisha vikwazo katika uuzaji wa bidhaa za chakula, na sasa soko la kimataifa linakabiliwa na upungufu wa bidhaa hizo.

 

Taarifa hiyo imesema kuwa, kutokana na vizingiti vinavyokwamisha kazi na biashara vinavyosababishwa na gonjwa wa COVID-19 (corona), zinapaswa kufanyika jitihada kubwa za kudhamini kazi za biashara na kuzuia uhaba wa bidhaa za chakula.

Mashirika ya UN: Corona itasababisha uhaba wa chakula

 

Wakuu wa jumuiya hizo tatu za Umoja wa Mataifa wamesema kuwa, matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vizuizi vya kusafirisha wafanyakazi wa sekta ya kilimo na chakula, na ucheleweshaji wa mpakani wa mashehena ya vyakula vinasababisha kuharibika kwa sehemu kubwa ya bidhaa hizo.

 

Maafisa wa nchi za Ulaya na Marekani pia wametahadharisha kuhusiana na athari mbaya za maambukizi ya virusi vya corona duniani. 

 

Maduka makubwa ya bidhaa yameonekana kuwa tupu katika nchi nyingi za Magharibi baada ya watu kumiminika katika maeneo hayo kwa ajili ya kununua bidhaa za dharura katika kipindi hiki cha kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon