Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 27.03.2020:


Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo mwenye miaka 30, amepewa ofa ya kuongezewa mkataba wa miaka miwili na timu yake ya China Shanghai Shenhua huku mshahara ukipanda mpaka paundi 400,000 kwa wiki.

Real Madrid wana nia ya kumsaini Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund msimu wa joto. Mshambuliaji huyo wa Norway kwenye mkataba wake kunakipengere cha kuuzwa kwa pauni 50m

Manchester United wanampango wa kumuongezea mkataba kiungo wake Paul Pogba, 27, Kiungo wa kati wa Uhispania Pedro, 32, ameweka wazi ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu wakati mkataba wake na Blues utakuwa umemalizika.

West Ham, Sporting Lisbon na Anderlecht ni kati ya vilabu vinavyo mtazama kipa wa Liverpool wa Ujerumani, Loris Karius, 26, ambaye yupo kwa mkopo Besiktas na anapatikana kwa pauni milioni 4.5 mwishoni mwa msimu.

Loris Karius

West Brom wanataka kumchukua moja kwa moja beki wa kati wa Croatia Filip Kronvinovic ambayo yupo kwa mkopo, ikiwa watarudi ligi kuu.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu