Vita dhidi ya corona; Ethiopia yawaachia huru maelfu ya wafungwa


Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa itawaachia huru maelfu ya wafungwa, ili kuzuia kuenea kwa kasi kirusi hatari cha corona nchini humo.

Adanech Abebe, Mwanasheria Mkuu wa Ethiopia amesema serikali itawaachia huru wafungwa zaidi ya elfu nne, aghalabu yao wakiwa wale waliokuwa wamefungwa kwa makosa madogo na wenye vifungo vya chini ya mwaka mmoja.

Amesema, "kutokana na kasi ya kuenea kwa kirusi cha corona, serikali kuanzia (leo) Alkhamisi itaanza kuwaachia huru wafungwa 4,011 ili kuondoa mrundikano na msongamano wa wafungwa katika magereza yetu."

Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya ya Umma ya Ethiopia, kesi 12 za ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na kirusi cha corona zilikuwa zimethibitishwa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kufikia Jumanne jioni. Hii ni baada ya kuwafanyia vipimo watu 480.

Amnesty International yataka wafungwa kuachiwa huru katika kipindi hiki cha kukabiliana na corona.

Alhamisi iliyopita, serikali ya Misri pia iliwaachilia huru wafungwa 15 wanachama wa vyama na makundi ya kisiasa ya wapinzani,

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limewataka viongozi wa Misri wawaachilie huru mara moja wafungwa wa kisiasa waliorundikana kwenye jela na magereza ya nchi hiyo bila ya masharti yoyote, ili kuokoa maisha yao kutokana na mlipuko wa corona.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu