Hospitali za Uingereza zakabiliwa na wakati mgumu kutokana na maambukizo ya corona

March 28, 2020

Mkuu wa Taasisi ya Hospitali nchini Uingereza ametahadharisha kuwa hospitali nchini humo zinakabiliwa na hali ngumu kutokana na kuongezeka watu walioambukizwa virusi vya corona.

 

Chris Hopson ametahadharisha kuwa hospitali nchini Uingereza zinalemewa na utendaji kazi kutokana na kuongezeka idadi ya wanaoambukizwa virusi vya corona, kasi ya maambukizo hali za wagonjwa pamoja na uhaba wa suhula za matibabu.

 

Mkuu huyo wa Taasisi ya Hospitali za Nchini Uingereza ameongeza kuwa uwezo  wa hospitali hizo wa kukabiliana na wimbi la wagonjwa wanaofika hospitalini ambao hali zao ni mbaya umefikia mwisho.  

Chris Hopson, Mkuu wa Taasisi ya Hospitali nchini Uingereza 

 

Hopson amesema kuwa wanaweza kuitaja hali hii ya sasa kama tsunami. Wakati huo huo Chris Hopson amemnukuu mkuu wa hospitali moja nchini Uingereza na kuongeza kuwa hospitali nchini humo zina hali mbaya kuliko ilivyodhaniwa.

 

Idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya corona inaongezeka kila siku huko Uingereza.

Hadi sasa watu 9,529 wameambukizwa virusi hivyo na tayari 465 wameaga dunia. Maafisa wa Wizara ya Afya ya Uingereza wanatabiri kuwa idadi ya mamabukizo na wanaoaga dunia kwa virusi vya corona nchini humo inatazamiwa kuongezeka pakubwa katika wiki zijazo.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon