Waziri wa Ulinzi wa Sudan afariki akiwa Juba, Sudan Kusini


Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Luteni Jenerali Jamaleldin Omar, amekufa kufuatia mshtuko wa moyo akiwa Sudan Kusini wakati akishiriki katika mazungumzo ya amani baina ya serikali na waasi mjini Juba.

Katika taarifa siku ya Jumatano, Jeshi la Sudan limesema, Omar alikuwa mwanachama wa baraza la kijeshi lilolochukua madaraka baada ya kupinduliwa Omar al Bashir mwaka uliopita.

Imedokezwa kuwa, Omar alishiriki katika mazungumzo yaliyoendelea hadi Jumanne usiku na aliaga dunia usiku wa kuamkia leo. Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu kifo cha waziri hiyo.

Mazungumzo ya wawakilishi wa serikali ya Sudan na viongozi wa makundi ya waasi yalianza upya katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba Oktoba mwaka jana.

Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Sudan Abdallah Hamdok

Mazungumzo hayo ya amani yalianza kufuatia mwito wa nchi za eneo kwa pande hizo kuonyesha nia ya kisiasa ya kutatua mgogoro ambao umekuwa ukitokota nchini humo kwa muda mrefu.

Wakati huo, serikali ya Sudan ilijipa miezi sita kufikia mkataba kamili wa amani. Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Sudan Abdallah Hamdok alisema kupata amani ya kudumu ni kipaumbele cha serikali anayoiongoza.

mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu