Watawala wa Marekani wanatumia corona kama fursa ya kuendeleza uhasama


Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza kuwa: "Watawala wa Marekani wanatumia corona kama fursa ya kuendeleza uhasama."

Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran katika ujumbe wa Twitter siku ya Jumanne ameandika kuwa, ni watawala wa Marekani pekee wanaotumia corona kama fursa ya kuendeleza uadui na kuongeza kuwa, furaha ya Waziri wa Biashara wa Marekani baada ya kuibuka ugonjwa wa corona China na kutaja ugonjwa huo kuwa ni wenye manufaa kwa uchumi wa Marekani, na pia pendekezo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo la kuhujumiwa Iran kijeshi, ni mifano ya wazi ya uadui huo.

Aidha amehoji, je, kirusi cha corona kimetokana na akili ya mtu gani punguani na mtenda jinai dhidi ya binadamu?

Kirusi cha corona ambacho rasmi kinajulikana kama COVID-19 kiliripotiwa kwa mara ya kwanza mwisoni mwa mwezi Disemba 2019 mjini Wuhan nchini China. Hadi sasa ugonjwa wa COVID-19 umeenea katika nchi 195 kote duniani na kuambukiza watu 392,000 ambapo miongoni mwao 102,000 wameandoka hospitalini baada ya kupata nafuu huku wengine 17,000 wakifariki dunia.

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu