Kauli potovu ya Trump kuhusu Chloroquine yapelekea Wanigeria kulazwa hospitalini


Raia wasiopungua watatu wa Nigeria wamelazwa hospitalini baada ya kumeza idadi kubwa ya tembe za Chloroquine, dawa ya kutibu ugonjwa wa malaria wakiwa na itikadi huwa dawa hiyo inaweza kutibu ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona.

Siku chache zilizopita, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Ikulu ya White House kuwa matokeo ya majaribio ya awali ya dawa ya Chloroquine katika kutibu virusi vya corona yameonekana kufanikiwa, na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDC) imeidhinisha matumizi ya Chloroquine katika kutibu ugonjwa huo.

Hata hivyo baadaye FDC ilitoa taarifa kupinga matamshi hayo ya Trump na kusema uchunguzi kuhusu uwezekano wa kutumia Chloroquine bado unaendelea na bado haijatoa idhini ya kutumika dawa hiyo.

Kufuatia kauli hiyo ya upotoshaji ya Trump, baadhi ya sehemu nchini Nigeria zimeshuhudia ongezeko la manunuzi ya dawa hiyo na kusababisha bei yake kupanda.

Gboyega Akosile, Msemaji wa Gavana wa Lagos amewatahadharisha watu kuhusu utumizi wa dawa hiyo iliyopendekezwa na Trump.

Meneja wa mradi wa operesheni za dharura wa Ofisi ya Shirika la Afya Duniani barani Afrika Michel Yao amesema, dawa takriban 20 ikiwemo Chloroquine zinafanyiwa majaribio ya kitabibu na nchi mbalimbali kwa ajili ya kuangalia ufanisi wa kutibu virusi vya Corona, na sasa ni mapema kuipendekeza dawa yoyote.

Taarifa zaidi zinasema wanandoa wenye umri wa miaka 60 jimboni Arizona Marekani nao pia walitumia Chloroquine kujikinga na virusi vya Corona, ambapo mume alifariki dunia na mke yupo mahututi akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi.

www.mzunguko.com

kutibu ugonjwa huo.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu