Malawi kufanya uchaguzi wa marudio Julai 2

Uchaguzi wa urais nchini Malawi unatarajiwa kurudiwa tena Julai 2, kufuatia amri ya mahakama ya juu nchini humo, baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika mwaka jana kufutwa kufuatia udanganyifu.

Uchaguzi wa urais nchini Malawi unatarajiwa kurudiwa tena Julai 2, kufuatia amri ya mahakama ya juu nchini humo, baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika mwaka jana kufutwa kufuatia udanganyifu, tume ya uchaguzi nchini humo imesema Jumatatu hii.

"Kufuatia maamuzi ya mahakama ya katiba ya Februari 3, yaliyofuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuagiza kufanyika uchaguzi mpya, kwa sababu ya dosari tunatangaza kwamba chaguzi zitafanyika Julai 2,” mwenyekiti wa tume hiyo Jane Ansah amewaambia mkutano wa waandishi wa habari.

Katika maamuzi ya kwanza kabisa kuwahi kufikiwa nchini humo, mahakama ilibatilisha matokeo ya uchaguzi wa Mei 21, yaliyomrejesha mamlakani kwa awamu ya pili rais Peter Mutharika.

Mahakama ilisema matokeo ya uchaguzi kwa kiasi kikubwa yaligubikwa na udanganyifu na hususan "matumizi makubwa ya wino mweupe wa masahihisho kwenye karatasi za kupigia kura”.

Iliagizwa kufanyika kwa chaguzi mpya katika kipindi cha siku 150, lakini Mutharika aliikatia rufaa maamuzi hayo. Rufaa yake hiyo itasikilizwa na mahakama ya juu Zaidi kuanzia Aprili 15.

Rais Mutharika hadi sasa bado hajakubali kusaini mapendekezo kuhusu mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yanayotaka mtu kupata wingi wa zaidi za asilimia 50 ili kuingia mamlakani kwa awamu ya pili.

Mapendekezo hayo ni kizingiti kikubwa kwa Mutharika, ambaye alitangazwa mshindi kwa ushindi wa asilimia 35.8 tu ya kura.

www.mzunguko.com

udanganyifu, tume ya uchaguzi nchini humo imesema Jumatatu hii.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu