Utafiti: Wanaume wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa corona kuliko wanawake

March 24, 2020

Utafiti mpya unaonesha kuwa, wanaume wanakabiliwa na hatari zaidi ya kuambukizwa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 zaidi ya wanawake.

 

Hayo yalisemwa jana Jumatatu na Nikolay Briko, Mkuu wa Idara ya Tiba ya Magonjwa ya Mripuko  katika Chuo Kikuu cha Moscow na afisa wa Wizara ya Afya wa Russia.

 

 

Amefafanua kuwa, “tukitazama nani anayepata virusi vipya vya corona, wanaume huambukizwa mara nyingi zaidi kushinda wanawake, karibu mara mbili zaidi. Sababu ya hali hii haijulikani. Huenda hii ni aina maalumu ya hali ya kinga ya mwili au sifa ya kinga ya jinsia ya kiume na kike."

 

Amesema haijabainika iwapo aina ya damu inaweza kuathiri uwezo wa mtu kupata ugonjwa huo au la, na kuongeza kuwa, kuna baadhi ya sifa za jeni zinazodhibiti uwezo na jinsi maambukizi yanavyokuwa.

 

Wanaume waathirika zaidi na corona kuliko wanawake

 

Afisa huyo wa Wizara ya Afya wa Russia ameeleza bayana kwamba, kiwango cha hatari cha ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona ni takriban asilimia 4.3.

 

Aghalabu ya nchi duniani zimeripoti kesi za maambukizi ya ugonjwa huo ulioanzia nchini China mwishoni mwa Disemba mwaka jana 2019.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon