Maandamano yanayosababishwa na Ugonjwa wa corona katika mji wa Hongkong


Virusi vya Corona ni kundi la virusi vinavyoweza kusababisha magonjwa kwa wanyama (mamalia na ndege) lakini pia kwa binadamu.

Inaaminiwa ni aina ya virusi vilivyohama kutoka kwa wanyama na kuathiri binadamu pia.

Nukuu Muhimu.

Virusi vya corona huwa na uwezo wa kubadilika na aina nyingi husababisha magonjwa yasiyo hatari sana upande wa binadamu.

Kudhoofika kwa mwili kutokana na mashambulio ya virusi kunafungua milango kwa bakteria wanaoleta maambukizo ya mfumo wa upumuo, kama mafua au homa ya mafua, yanayoishia kwa kawaida baada ya siku kadhaa, lakini kuna pia maambukizo ya hatari yanayoweza kusababisha kifo.

Hakuna chanjo au dawa ya kudhibiti virusi vya aina hii. Kwa hiyo uponyaji hutegemea mara kwa mara nguvu ya kinga mwilini cha kila mtu. Hii inamaanisha virusi hivi huleta hatari hasa kwa watu wenye kinga cha mwili kilichodhoofishwa.

Aina hizo za virusi zina uwezo wa kubadilika, miaka ya nyuma ulikuwa na mabadiliko kadhaa yaliyosababisha vifo vya watu na kuenea haraka kimataifa, hivyo kusababisha hofu za epidemiki au hata pandemia.

www.mzunguko.com

Virusi vya Corona vipo vya aina mbalimbali, zikiwemo 229E, NL63, OC43, HKU1 na Covid-19.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu