Wanawake 10 watengeneza filamu toka Afrika kupata mafunzo kwa msaada wa UNESCO


Audrey Azoulay

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Audrey Azoulay na mtayarishashi filamu mashuhuri kutoka Japan NaomiKawase wametangaza majina 10 ya washindi wa tuzo ya UNESCO kwa ajili ya watayarishaji vijana wa filamu ambao ni wanawake toka barani afrika.

NaomiKawase

Tangazo hilo limetolewa kandoni mwa kikao cha 13 cha kamati ya kimataifa ya mkataba kuhusu ulinzi na uchagizaji wa tamaduni tofauti kinachofanyika mjini Paris Ufaransa.

Akizungumzia tangazo hilo Bi. Azoulay amesema “Ni muhimu kwa sekta ya filamu kufanya sauti za Afrika zisikike ili kusaidia kuibua ukuaji wa tamaduni tofauti , kuweka mawazo mapya na hisia, na kuhakikisha kwamba wanawake kama watayarishaji wanachangia katika majadiliano muhimu ya kimataifa kwa ajili ya amani, utamaduni na maendeleo.”

Wanawake hao 10 watayarishaji wa filamu wenye umri wa kati ya miaka 21 hadi 35 kutoka Burkina Faso, Kenya, Senegal na Afrika Kusini watakuwa mafunzoni katika makazi ya Tawara katika mkoa wa Nara, kuanzia tarehe 29 Machi hadi 12 Aprili mwaka huu.

Watapatiwa mafunzo na Bi. Kawase na mtayarishaji filamu kutoka Senegal Fatou Kande Senghor. Mradi huo unaungwa mkono na serikali ya Japan na wakfu wa Japan.

Bi.Kawase anasema kwa upande mmoja “kuwa mwanamke ilifanya kuwa rahisi kwangu kuangalia kwa karibu mazingira yangu , sio kuwa katika ulingo au kuwa kinara, wanawake wanaweza kufanya mapinduzi mapya. Kwa upande wangu naandaa vitu kutokana na vyanzo vyangu mwenyewe. Naamini kuna kitu cha kimataifa katika uzoefu wangu binafsi”

www.mzunguko.com

ilijulikanayo kama Nara Residency for Young African Female Filmmakers.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu