Saudia yaanzisha wimbi jipya la kuwatia mbaroni Wapalestina

February 14, 2020

 

Utawala wa Aal-Saud umeanzisha wimbi jipya la kuwakamata na kuwazuia raia wa Palestina wanaoishi Saudi Arabia kwa madai ya kuiunga mkono Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).

 

Shirika la Wafungwa wa Itikadi (Prisoners of Conscience), asasi isiyo ya kiserikali inayopigania haki za wafungwa wa Kipalestina nchini Saudia limesema Wapalestina kadhaa wakiwemo watu wa familia za raia wa Palestina waliokamatwa na kuwekwa korokoroni tangu Aprili mwaka jana wametiwa mbaroni na watawala wa Riyadh katika wimbi jipya la kamatakamata.

 

 

Ofisi ya Uhusiano wa Kitaifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuendelea kukamatwa na kufungwa jela nchini Saudia raia wa Palestina ni jambo lisilokubalika.

 

Hamas inasema Wapalestina ambao wametiwa nguvuni huko Saudia tangu kuanza mwaka huu wa 2019 wanakabiliwa na mateso na kuhojiwa katika mazingira magumu. Abu Zuhri amesisitiza kuwa, baadhi ya Wapalestina waliotiwa mbaroni wamehojiwa na watu kutoka nje ya nchi

Muhammad al Khidr, afisa wa Hamas aliyerejeshwa jela Saudia baada ya kutolewa hospitalini

 

Kufikia mwishoni mwa mwaka jana, kulikuwa na jumla ya Wapalestina 60 korokoroni nchini Saudi Arabia; baadhi yao wakiwa ni wanachama au waungaji mkono wa harakati ya Hamas. Kadhalika baadhi ya raia hao wa Palestina wameishi Saudia kwa zaidi ya miaka 30.

 

Miongoni mwa Wapalestina waliotiwa nguvuni nchini Saudi Arabia ni Abu Ubaydah al-Agha, mwanachama wa ngazi ya juu wa Hamas pamoja na mwenzake Muhammad al-Khidr ambaye anaishi nchini Saudi Arabia kwa karibu miaka 30 sasa. 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon