Kumbukumbu ya kihistoria ya siku ya wapendanao[Valentine day]

February 14, 2020

Siku ya wapendanao (Valentine's Day) ni sikukuu ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari ya kila mwaka.

 

Historia yake imeanzia karne ya 3 huko Roma ambapo kulikuwa na padri mmoja aliyeitwa  Valentinus ambaye akaja kuheshimiwa kama matakatifu hasa tarehe   hiyo.

 

Mt. Valentinus akimbatiza Mt. Lusila,

 

Valentinus (Terni, Italia, 176 hivi - Roma, 14 Februari 273) alikuwa askofu wa Terni.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini katika Kanisa Katoliki, lakini pia na Waorthodoksi, Waanglikana na Walutheri kadhaa.

 

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Februari ya kila mwaka.

Valentinus anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani kama Valentine's Day.

 

Historia yake inawezekana inamchanganya na Valentinus mwingine, padri wa karne ya 3 huko Roma, aliyeuawa mwaka 269 katika mazingira yaleyale.

 

Kuna hadithi mbalimbali juu yake. Mojawapo inasema Valentinus aliandika barua kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.

 

Mbali ya hadithi hiyo , askofu huyo alijulikana kwa miujiza yake. Huko Terni, mnamo 2011, ilipatikana mifupa ya Sabino  na Serapia: mmoja alikuwa Mpagani akida wa jeshi la Roma, mwingine msichana Mkristo motomoto.

 

Kwa ajili yake Sabino aliongokea Ukristo, lakini baada ya muda mfupi aligundua kwamba Serapia ni mgonjwa wa kifua kikuu. Ili asitengane naye, Sabino alimuomba Valentinus awabariki , naye alibariki ndoa yao na kuomba mapendo yao yadumu milele. Baadaye walifariki pamoja wamekumbatiana na ndivyo mifupa yao inavyopatikana hadi leo.

 

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon