Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Museveni kuwakutanisha ana kwa ana Rais wa Sudan Kusini na Machar

November 5, 2019

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anatazamiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa ana kwa ana baina ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na kinara wa upinzani Riek Machar jijini Kampala.

 

Kikao hicho cha leo ni cha tatu cha ana kwa ana baina ya mahasimu hao wawili wa kisiasa wa Sudan Kusini, chini ya upatanishi wa Rais Museveni.

 

Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito Sudan Abdel Fattah Al Burhan pia anatazamiwa kushiriki mazungumzo hayo ya amani, ili kutafutia ufumbuzi utesi uliopo kabla ya kuundwa serikali mpya ya muungano Novemba 12.

 

Haya yanajiri siku chache baada ya Machar kuuambia ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuwa hatashiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa itakayoundwa mwezi huu nchini humo.

Kiir na Machar katika kikao cha Juba chini ya upatanishi wa Museveni na Omar al-Bashir.

 

Anadai kuwa pande husika katika mgogoro wa Sudan Kusini zimeshindwa kufikia makubaliano juu ya jinsi ya kuliunganisha jeshi la nchi hiyo suala ambalo ni sharti muhimu katika makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka jana; kwa msingi huo hakuna uwezekano wa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.

 

Mwezi Mei mwaka huu pande mbili hasimu nchini Sudan Kusini zilitia saini makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika kipindi cha miezi sita ijayo na kuunda serikali ya mpito hadi kufikia tarehe 12 Novemba.

 

Sudan Kusini ilitumbukia katika vita vya ndani Disemba 2013 baada ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar wa kabila la Nuer kwamba alihusika na jaribio la kuipindua serikali yake.

 

www.mzunguko.com

 

 

 

 

 

 

 

 

Share on Facebook
Share on Twitter
Please reload