Zimbabwe yaonya kuhusu matamshi ya uingiliaji mambo ya balozi wa Marekani


Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe amemuonya balozi wa Marekani mjini Harare, mji mkuu wa nchi hiyo kutokana na matamshi yake ya uingiliaji katika masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Sibusiso Moyo amesema kuwa, iwapo Brian Nichols, balozi wa Marekani mjini Harare ataendelea kutoa matamshi ya uingiliaji katika masuala ya ndani ya Zimbabwe na kuchochea wapinzani dhidi ya serikali, basi atafukuzwa nchini humo. Itakumbukuwa kuwa wiki iliyopita balozi huyo wa Marekani alinukuliwa akisema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Zimbabwe havijahusika na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo, bali hali hiyo inatokana na uongozi mbaya.

Kwa mujibu wa Brian Nichols uongozi mbaya wa watawala ndio sababu ya hali mbaya inayoshuhudiwa nchini humo. Hii ni katika hali ambayo Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea Zimbabwe vikwazo tokea miaka 20 iliyopita.​

www.mzunguko.com


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu